Galatians 3:1-6

Imani Au Kushika Sheria?

1 aNinyi Wagalatia wajinga! Ni nani aliyewaroga? Isa Al-Masihi aliwekwa wazi mbele yenu kwamba amesulubiwa. 2 bNataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia? 3 cJe, ninyi ni wajinga kiasi hicho? Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kumalizia katika mwili? 4 dJe, mlipata mateso kiasi hicho bure? Ni kama kweli yalikuwa bure! 5 eJe, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?

6 fKama vile “Ibrahimu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.”
Copyright information for SwhKC